Friday, October 30, 2009

ALBINOS IN TANZANIA

Anthony Komanya
Oktoba 30,2009

UMASKINI CHANGAMOTO MAUAJI YA ALBINO TANZANIA

"Watu watatu wahukumiwa kifo",taarifa katika wavuti wa BBC News Africa chini ya kichwa cha habari 'Death For Tanzania Albino Killers', inavuta hisia ya walimwengu.

Ni kufuatia Mahakama kuu maalumu kaskazini magharibi mwa Tanzania, katika mkoa wa Shinyanga kutoa hukumu ya kifo kwa watu watatu kwa kuthibitika kumwuua albino.

Kwa mujibu wa taarifa hizo wamehukumiwa kunyongwa kwa kosa la kumwua mtoto wa kiume albino Matatizo Dunia(14)kwa kumshambulia, kumwua na kisha kumkata miguu yake na kutokomea nayo katika wilaya ya Bukombe iliyopo mkoani Shinyanga.

"Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, Maalibino wapatao 25, wakiwemo watoto wametendewa ukatili ikiwemo kunyofolewa viungo na kuuawa nchini Tanzania" wavuti ya ALJazeerEnglish,inaitaarifu dunia katika taarifa zake za June 25 2008.

Katika Siku za hivi karibuni maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Zeruzeru) maarufu kama 'Albino' yamekuwa katika hali tete na kujaa simanzi.

Ghafla jamii imeanza kutambua uwepo wao na kuwabaini kwa mwonekano na nia 'mkengeuko' tofauti na watu walicvyoiona na kuitambua jamii ya maalbino tangu zamani kale.

Mapokeo yanatanabaisha kwamba katika imani za jamii nyingi za Kiafrika wakiwemo baadhi ya watanzania, ilikuwa nuksi kwa familia kupata mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, maarufu kwa jina hilo la Zeruzer(Albino).

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Mstaafu, Yohana Balele,wakati akiongea na jamii kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Familia Duniani, katikati ya mwaka huu mjini Shinyanga, anakumbusha:

"Baadhi ya makabila mtoto mwenye ulemavu huo akizaliwa katika familia wazazi walichukua hatua za kummaliza kabla hajaonekana na watu wengine nje ya familia hiyo".

Anaendelea kusema kwamba hata hivyo imani hiyo haikusababisha wimbi la mauaji ya albino waliopata kuishi mpaka hadi utu uzima na hata waliofanya usiri huo siyo wengi na waliofanya hivyo ni kwa kujificha katika uvuli wa 'mimba imeharibika'tofauti na sasa.

Kufuatia hukumu hiyo kasikazini magharibi mwa Tanzania, baadhi ya watu wamekuwa na mawazo kwamba hukumu hiyo itawatia hofu wenye nia ya kutenda kosa hilo na hivyo kumaliza kabisa tatizo hilo la aibu.

Mwandishi wa wavuti ya BBC AFRICA, Mary Haper, ana maoni tofauti akidai,"In a country as poor as Tanzania, it is likely that some murders will continue because so much money can be made from selling the body parts".

Rai hii inaelekeza jamii ya watu duniani kukazia dhana nzima ya tatizo hili kwenye 'Uchumi'.

Wanaowinda watu wenye ulemavu wanasukumwa na hali ya uhitaji wa kupata fedha, hata kama wao wenyewe hawana imani ya dhana anayotajwa tajwa kuwa viungo hivyo hubeba nguvu za giza (ushirikina) hadi kuwezesha upatikanaji wa fedha maradufu.

Viungo vya albino hutumiwa katika dawa zinazotumiwa na baadhi ya waganga wa kienyeji wakiwaahidi wateja wao kupata utajiri

Mwezi March mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete katika dhamira ya kukomesha kabisa mauaji hayo ya aibu, akawaita Watanzania kujitokeza kwenye zoezi la upigaji kura za kuwafichua wanaodhaniwa kuwa kwenye kundi hilo la uhalifu.

Watuhumiwa wengi wametiwa mbaroni, ingawa zoezi zima la utoaji haki stahiki linaonekana kwenda mwendo wa taratibu sana.

Aidha sambamba na wito huo wa Mkuu wa taifa la Watanzania, serikali kupitia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, nayo kwa upande wakde ikapiga marufuku vibali vya waganga wa jadi ikawataka waombe upya vibali hivyo.

"The Tanzanian government has publicly stated its desire to end the killings,
in March, President Jakaya Kikwete called on Tanzanians to come forward with any information they might have", anaeleza Juliet Lapidos, katika taarifa kupitia wavuti BBC NEWS AFRICA (Albino Africans lives in fear after witch doctor butchery}

Kwa mujibu wa wavuti hiyo Uongozi wa serikali ya Tanzania unadai kuwa waganga wa jadi (kienyeji) wanahusika katika kusababisha wimbi hili la uhalifu.


"Tumekuwa na kawaida ya kuelekezea lawama waganga wa jadi tukasahau hata kuchimba zaidi ili tuweze kuona chanzo cha tatizo", anaonya Mzee mmoja mstaafu wa utumishi wa umma.

Anaendelea kukumbusha kukengeuka huko kuwa kumeanza na dhana ya mauaji ya vikongwe nchini hususan katika mikoa ya kanda ya ziwa.

"Mwanasiasa fulani nadhani, siku moja huko nyuma alikwea jukwaani na kuanzisha dhana ya 'macho menkundu' kuhusia=shwa na mauaji ya vikongwe", anashangaa mzee huyo, akiendelea kudai kuwa siyo kweli kwamba mauaji yote yanatokana na imani za ushirikina'.

"Mengi zaidi hutokana na kisasi, ugomvi wa mashamba, urithi siyo uchawi".

Changamoto kubwa kwa watanzania ni kuweka mikakati madhubuti ya kuondoa umaskini kwa wananchi wake kwa kupitia uboreshaji wa matumizi ya rasilimali watu na mazingira yake, haya ndiyo mawazo ya mzee huyu.

Mwisho

.

No comments:

Post a Comment