Wednesday, October 28, 2009

INTERNATE CHOMBO MUHIMU KWA MWANDISHI

Anthony Komanya
Mafunzo ya Internate
Oktoba 28,2009

(SIKU YA TATU)

INTERNATE KAMA CHOMBO MUHIMU KWA MWANDISHI

IMEELEZWA kwamba teknolojia mpya ya Internate imeongeza marudufu fursa ya upatikanaji wa habari za dunia yote kwa mwandishi wa habari.

Ni kutokana na mwandishi anayetumia mtandao huo kuwa na fursa ya kufungua na kusoma chochote kinachoandikwa na media zingine na kuzitumia kama chanzo chake cha habari.

Kwa mujibu wa Mkufunzi wa mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Chuo cha Banki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza, Peik Johansson, katika mkusanyiko wa magazeti na taarifa zingine za kidunia mwandishi anaweza kutafiti ili kupata uhalisia wa taarifa za eneo husika anazotoa.

Katika mazoezi yaliyofanyika kuthibitisha ukweli huu, washiriki wa mafunzo walitembelea wavuti za 'media' mbalimbali kama vile ippmedia, darhotiwire, mwananchi, habari leo, star tv na janmii kwanza.

Aidha, washiriki wa mafunzo wameingia katika wavuti zingine kama vile Jamii forum (Mwnakijiji), Daily monitor, Daily news, Mail Gurdian (Afrika ya Kusini), All Africa forum na zingine nyingi walizotembelea.

Katika hatua nyingine washiriki waliangalia mawasiliano ya barua pepe (e-mail) kama chombo muhimu kwa Mwandishi wa habari kwa kutuma taarifa kama njia ya mawasiliano ya haraka, kufanya mahojiano na vyanzo vya habari na kufanya utafiti katika kutafuta ukweli na hali halisi.

Changamoto za matumizi ya barua pepe zilibainishwa zikiwemo namna anavyopaswa kuandika kwa kutumia kauli fupi zenye kujitosheleza na kila para iwakilishe 'topic' kamili, kuchagua dhamira (wazo) mahiri, na kusoma tena na tena alichokiandika kabla ya kukituma.

Ujangili (plagiarism) wa habari za mwandishi mwingine nao umebainishwa katika mada kuwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za Kimataifa (http portalunesco.org) na kwamba mwandishi wa habari asishawishike kufanya hivyo.

Ilifahamishwa kuwa siku za hivi karibuni kosa hili limekuwa rahisi sana kutendeka kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya kompyuta na internate.

Kwa mujibu wa Johnsson, awali mwizi kama huyo alipaswa kwenda kwenye maktaba kusoma na kuiba taarifa husika.


Washiriki wameshauriwa kutembelea wavuti ya 'plagiarism.org' ili kuona makosa yaliyoorodheshwa ambayo yanayotokana na uvunjaji wa kanuni hii.

"Kunukuu kwa uhakika vyanzo vya habari ni njia pekee kwa mwandishi wa habari kukwepa kuingia katika kashfa hii", alisisitiza Johansson.

Kama ilivyo ada, umuhimu wa mafunzo haya unaendelea kudhihirika kila yanapoendelea, nafikiri mpaka yatakapofikia hatima nitakuwa na weledi katika masuala na matumizi ya 'Internate' kwa shughuli zangu za uandishi.


asanteni

No comments:

Post a Comment