Friday, October 30, 2009

ALBINOS IN TANZANIA

Anthony Komanya
Oktoba 30,2009

UMASKINI CHANGAMOTO MAUAJI YA ALBINO TANZANIA

"Watu watatu wahukumiwa kifo",taarifa katika wavuti wa BBC News Africa chini ya kichwa cha habari 'Death For Tanzania Albino Killers', inavuta hisia ya walimwengu.

Ni kufuatia Mahakama kuu maalumu kaskazini magharibi mwa Tanzania, katika mkoa wa Shinyanga kutoa hukumu ya kifo kwa watu watatu kwa kuthibitika kumwuua albino.

Kwa mujibu wa taarifa hizo wamehukumiwa kunyongwa kwa kosa la kumwua mtoto wa kiume albino Matatizo Dunia(14)kwa kumshambulia, kumwua na kisha kumkata miguu yake na kutokomea nayo katika wilaya ya Bukombe iliyopo mkoani Shinyanga.

"Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, Maalibino wapatao 25, wakiwemo watoto wametendewa ukatili ikiwemo kunyofolewa viungo na kuuawa nchini Tanzania" wavuti ya ALJazeerEnglish,inaitaarifu dunia katika taarifa zake za June 25 2008.

Katika Siku za hivi karibuni maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Zeruzeru) maarufu kama 'Albino' yamekuwa katika hali tete na kujaa simanzi.

Ghafla jamii imeanza kutambua uwepo wao na kuwabaini kwa mwonekano na nia 'mkengeuko' tofauti na watu walicvyoiona na kuitambua jamii ya maalbino tangu zamani kale.

Mapokeo yanatanabaisha kwamba katika imani za jamii nyingi za Kiafrika wakiwemo baadhi ya watanzania, ilikuwa nuksi kwa familia kupata mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, maarufu kwa jina hilo la Zeruzer(Albino).

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Mstaafu, Yohana Balele,wakati akiongea na jamii kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Familia Duniani, katikati ya mwaka huu mjini Shinyanga, anakumbusha:

"Baadhi ya makabila mtoto mwenye ulemavu huo akizaliwa katika familia wazazi walichukua hatua za kummaliza kabla hajaonekana na watu wengine nje ya familia hiyo".

Anaendelea kusema kwamba hata hivyo imani hiyo haikusababisha wimbi la mauaji ya albino waliopata kuishi mpaka hadi utu uzima na hata waliofanya usiri huo siyo wengi na waliofanya hivyo ni kwa kujificha katika uvuli wa 'mimba imeharibika'tofauti na sasa.

Kufuatia hukumu hiyo kasikazini magharibi mwa Tanzania, baadhi ya watu wamekuwa na mawazo kwamba hukumu hiyo itawatia hofu wenye nia ya kutenda kosa hilo na hivyo kumaliza kabisa tatizo hilo la aibu.

Mwandishi wa wavuti ya BBC AFRICA, Mary Haper, ana maoni tofauti akidai,"In a country as poor as Tanzania, it is likely that some murders will continue because so much money can be made from selling the body parts".

Rai hii inaelekeza jamii ya watu duniani kukazia dhana nzima ya tatizo hili kwenye 'Uchumi'.

Wanaowinda watu wenye ulemavu wanasukumwa na hali ya uhitaji wa kupata fedha, hata kama wao wenyewe hawana imani ya dhana anayotajwa tajwa kuwa viungo hivyo hubeba nguvu za giza (ushirikina) hadi kuwezesha upatikanaji wa fedha maradufu.

Viungo vya albino hutumiwa katika dawa zinazotumiwa na baadhi ya waganga wa kienyeji wakiwaahidi wateja wao kupata utajiri

Mwezi March mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete katika dhamira ya kukomesha kabisa mauaji hayo ya aibu, akawaita Watanzania kujitokeza kwenye zoezi la upigaji kura za kuwafichua wanaodhaniwa kuwa kwenye kundi hilo la uhalifu.

Watuhumiwa wengi wametiwa mbaroni, ingawa zoezi zima la utoaji haki stahiki linaonekana kwenda mwendo wa taratibu sana.

Aidha sambamba na wito huo wa Mkuu wa taifa la Watanzania, serikali kupitia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, nayo kwa upande wakde ikapiga marufuku vibali vya waganga wa jadi ikawataka waombe upya vibali hivyo.

"The Tanzanian government has publicly stated its desire to end the killings,
in March, President Jakaya Kikwete called on Tanzanians to come forward with any information they might have", anaeleza Juliet Lapidos, katika taarifa kupitia wavuti BBC NEWS AFRICA (Albino Africans lives in fear after witch doctor butchery}

Kwa mujibu wa wavuti hiyo Uongozi wa serikali ya Tanzania unadai kuwa waganga wa jadi (kienyeji) wanahusika katika kusababisha wimbi hili la uhalifu.


"Tumekuwa na kawaida ya kuelekezea lawama waganga wa jadi tukasahau hata kuchimba zaidi ili tuweze kuona chanzo cha tatizo", anaonya Mzee mmoja mstaafu wa utumishi wa umma.

Anaendelea kukumbusha kukengeuka huko kuwa kumeanza na dhana ya mauaji ya vikongwe nchini hususan katika mikoa ya kanda ya ziwa.

"Mwanasiasa fulani nadhani, siku moja huko nyuma alikwea jukwaani na kuanzisha dhana ya 'macho menkundu' kuhusia=shwa na mauaji ya vikongwe", anashangaa mzee huyo, akiendelea kudai kuwa siyo kweli kwamba mauaji yote yanatokana na imani za ushirikina'.

"Mengi zaidi hutokana na kisasi, ugomvi wa mashamba, urithi siyo uchawi".

Changamoto kubwa kwa watanzania ni kuweka mikakati madhubuti ya kuondoa umaskini kwa wananchi wake kwa kupitia uboreshaji wa matumizi ya rasilimali watu na mazingira yake, haya ndiyo mawazo ya mzee huyu.

Mwisho

.

Wednesday, October 28, 2009

INTERNATE CHOMBO MUHIMU KWA MWANDISHI

Anthony Komanya
Mafunzo ya Internate
Oktoba 28,2009

(SIKU YA TATU)

INTERNATE KAMA CHOMBO MUHIMU KWA MWANDISHI

IMEELEZWA kwamba teknolojia mpya ya Internate imeongeza marudufu fursa ya upatikanaji wa habari za dunia yote kwa mwandishi wa habari.

Ni kutokana na mwandishi anayetumia mtandao huo kuwa na fursa ya kufungua na kusoma chochote kinachoandikwa na media zingine na kuzitumia kama chanzo chake cha habari.

Kwa mujibu wa Mkufunzi wa mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Chuo cha Banki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza, Peik Johansson, katika mkusanyiko wa magazeti na taarifa zingine za kidunia mwandishi anaweza kutafiti ili kupata uhalisia wa taarifa za eneo husika anazotoa.

Katika mazoezi yaliyofanyika kuthibitisha ukweli huu, washiriki wa mafunzo walitembelea wavuti za 'media' mbalimbali kama vile ippmedia, darhotiwire, mwananchi, habari leo, star tv na janmii kwanza.

Aidha, washiriki wa mafunzo wameingia katika wavuti zingine kama vile Jamii forum (Mwnakijiji), Daily monitor, Daily news, Mail Gurdian (Afrika ya Kusini), All Africa forum na zingine nyingi walizotembelea.

Katika hatua nyingine washiriki waliangalia mawasiliano ya barua pepe (e-mail) kama chombo muhimu kwa Mwandishi wa habari kwa kutuma taarifa kama njia ya mawasiliano ya haraka, kufanya mahojiano na vyanzo vya habari na kufanya utafiti katika kutafuta ukweli na hali halisi.

Changamoto za matumizi ya barua pepe zilibainishwa zikiwemo namna anavyopaswa kuandika kwa kutumia kauli fupi zenye kujitosheleza na kila para iwakilishe 'topic' kamili, kuchagua dhamira (wazo) mahiri, na kusoma tena na tena alichokiandika kabla ya kukituma.

Ujangili (plagiarism) wa habari za mwandishi mwingine nao umebainishwa katika mada kuwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za Kimataifa (http portalunesco.org) na kwamba mwandishi wa habari asishawishike kufanya hivyo.

Ilifahamishwa kuwa siku za hivi karibuni kosa hili limekuwa rahisi sana kutendeka kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya kompyuta na internate.

Kwa mujibu wa Johnsson, awali mwizi kama huyo alipaswa kwenda kwenye maktaba kusoma na kuiba taarifa husika.


Washiriki wameshauriwa kutembelea wavuti ya 'plagiarism.org' ili kuona makosa yaliyoorodheshwa ambayo yanayotokana na uvunjaji wa kanuni hii.

"Kunukuu kwa uhakika vyanzo vya habari ni njia pekee kwa mwandishi wa habari kukwepa kuingia katika kashfa hii", alisisitiza Johansson.

Kama ilivyo ada, umuhimu wa mafunzo haya unaendelea kudhihirika kila yanapoendelea, nafikiri mpaka yatakapofikia hatima nitakuwa na weledi katika masuala na matumizi ya 'Internate' kwa shughuli zangu za uandishi.


asanteni

WAANDISHI WACHUKUA AKAUNTI YA BLOGGER

Anthony Komanya
Mafunzo ya Internate kwa Waandishi
Oktoba 27,2009

WAANDISHI KANDA YA ZIWA SASA 'BLOGGERS'

Imeelezwa kwamba matumizi ya Internate kupitia tovuti ya www.blogspot.com yamefanikiwa kusogeza na kuweka dunia mkononi mwa mwandishi wa habari ili atumie taarifa kama atakavyo katika wajibu wake kwa jamii.

Akitoa mada ya 'Internate inavyofanikiwa kubadili jamii duniani' Mkufunzi wa mafunzo hayo, Peik Johnsson, alifanikiwa kuthibitisha umuhimu kwa waandishi wa habri kutumia tovuti hiyo katika wajibu wao wa kuhabarisha jamii.

Alieleza kuwa kupitia tovuti hii katika Internate, mtu ataweza kuingia kwenye kurasa za website nyingine nyingi zenye manufaa makubwa katika shughuli za uandishi wa habari.

Baadhi ya website hizo ni pamoja na www.wikipedia.org (on line) ambayo ni kama kitabu cha dunia (encyclopedia) kilicho wazi kwa mtu yeyote kusoma na hata kuhariri kwa mahitaji yake ya upashanaji habari.

Wavuti hii inampa mwomba huduma ya internate fursa ya kuchagua lugha anayotaka kutumia kwani ina tafsiri za lugha nyingi kutoka kote duniani (Kiswahili kikiwemo)

Website nyingine iliyohamasisha waandishi wa habari kujiunga na akaunti ya 'blogger' ni ile ya www.ebay.com inayopatikana kwenye tofuti hiyo.

Kwa mujibu wa Johansson, 'ebay.com' ni sawa na duka la kidunia, ambamo mtu huweza kutumia kwa kununua vitu mbalimbali vikiwamo, nguo kuukuu na mpya, magari makuukuu na mapya, nyumba, kamerasiliana na bainisha kuwa kutokana na tovuti hiyo dunia yote inakuwa karibu na mwandishi mhusika wakati wowote.

Ukweli uliowazi ni kwamba, mafunzo haya yana faida kubwa na kwa mwandishi kuwa na 'blogger' ni kama kuingia katika maktaba ambamo kila kitu na taarifa anayohitaji anaweza kuipata.

Asante

Tuesday, October 27, 2009

Anthony Komanya
Oktoba 26,2009


Siku ya kwanza ya Mafunzo.

Tumeanza kwa kujitambulisha na kila mmoja kueleza uzoefu wake katika masuala ya Mtandao (Internate)

Tukaendelea tukiongozwa na mkufunzi Bw. Peik Johansson, kufuatilia kwa kina maana halisi ya Internate na matumizi yake katika nchi mbalimbali ulimwenguni.

Tulibaini kwamba ‘Internate’ ni njia inayotumika katika kutafuta habari, kutafiti taarifa mbalimbali, ni kama chumba cha habari na maktaba ya kidunia kwa waandishi na watafiti mbalimbali wa masuala ya kijamii.

Internate ni kama kitabu kikuu (Encyclopedia) cha ulimwengu kwa jamii. Ni mchakato na njia ya kisasa ya mawasiliano na kwamba ilianza kutumika mwaka 1957 kufuatia kurushwa kwa Satelite ya Warusi.

Matumizi ya Website katika Internate yalianza mwaka 1991 ambapo wasomi wawili waliianzisha kwa kutumia ‘hypernext makeup language’.

Tuliendelea kutafuta aina tofauti za Internate, kama vile Mikward Journalism on line, speat-type massage, reach-bath global and yet personal.

Katika hizo matumizi ya E-mail (multipurpose, responsiveness, na many receivers hutumika). Ingine ni Website, inayohusisha makampuni, ngo’s mitandao na shughuli mbalimbali za kijamii kama vile michezo.

Wakati wa mchana, tuliingia katika zoezi la matumizi ya Internate kununua tiketi kwa kwa usafari wa kimataifa.

Msafiri wa kwanza angeanza safari yake Helinsnki kuelekea Turku nchini Finland, kwa Ndege namba 135.. Msafiri mwingine angeanza safari yake Daresalaamu kwenda Bujumbura kwa kutumia Kenya Airways.

Changamoto: Binafsi sijafuata programu nyingine ya mafunzo ya matumizi ya Kompyuta na Internate tofauti na yale ya awali ya kutambulisha tekinolojia hii mpya. Hatua hii imekuwa ya mbele zaidi, hata hivyo ni changamoto kwangu kutia bidii.

Asanteni.